Tuesday, 14 November 2017

ulimwengu wa soka Tz

Sports update Gianluigi Buffon amesema timu ya Taifa ya Italia imeiangusha nchini nzima ya Italia kwa kushindwa kufuzu kucheza Fainali za Kombela Dunia baada ya kupoteza kwa 1-0 dhidi ya Sweden kwa jumla ya mechi mbili. Na Buffon mwenye umri wa miaka 39 ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka la kimataifa baada ya Azzurri kushindwa kupata matokeo katika dimba la San Siro. Buffon aliyekuwa kwenye hisia kali amesema,:" Sijipi pole peke yangu bali kwa soka zima la Italia. Tumefeli kitu ambacho pia kina maana kubwa sana katika ngazi ya kijamii. Kuna majuto ya kumaliza kama hivi, sio kwasababu muda huwa unapita." " Wote waliocheza wanajua ni jinsi gani hizi mechi zinavyokuwa ngumu . Tulishindwa kujionyesha kwa ubora wetu . Tulikosa utulivu wa kufunga magoli " " Tuna nguvu, kiburi na ukaidi . Tunajua jinsi gani ya kuinuka tena kama tunavyofanyaga mara nyingi. Naondoka katika kikosi cha Italia ambacho kinajua jinsi gani ya kuongea chenyewe. Kumbatio kwa kila mtu hasa ambao nimekuwa nao kwenye safari nzuri kama hii kwa muda mrefu." "Lawama lazima ziwe kwa kila mtu, Hakutakiwa kuwe na mbuzi wa kafara . Tunashinda pamoja, Tunafungwa pamoja."

0 coment�rios: