Thursday, 16 November 2017

ulimwengu wa soka Tz

Jose Mourinho ameiambia Sky Sports kwamba Zlatan Ibrahimovic atarejea dimbani ndani ya kikosi cha United kabla ya mwisho wa mwaka. Straika huyo ambaye aliumia goti mwishoni mwa msimu uliopita huenda akawa fiti kucheza kwenye mechi dhidi ya Manchester City , Old Trafford mwezi Ujao. Wakati huo huo gazeti la The Sun limeripoti kwamba yeye na Paul Pogba wapo njiani kucheza dhidi ya Newcastle United siku ya Jumamosi, Novemba 18. Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 35 ambaye alirejea mazoezini katika viwanja vya Carrington mwezi Oktoba na Mourinho amesema kwamba alikuwa na " hisia " Zlatan atarejea dimbani kabla ya mwisho wa 2017. " Yeye ni simba , ni mpiganaji , nafikiri hayo ni maelezo sahihi kuhusu Ibrahimovic, ana hasira ndani yake muda wote na hiyo ndio sababu kwanini anakaribia kurejea." " Kama tulivyotegemea , amepunguza muda wa kupona , kama tulivyokuwa tunasema wiki kadhaa zilizopita, atarejea mwaka 2017 , kitu ambacho ni uponaji wa ajabu sana." Ibrahimovic ambaye alikuwa mfungaji bora wa Man United msimu uliopita akifunga magoli 28 katika mashindano yote , alisaini mkataba wa mwaka mmoja mwezi Agosti na alijumuishwa kwenye kikosi cha UEFA cha hatua ya makundi.

0 coment�rios: